Unknown Unknown Author
Title: BENKI YA KIISLAM YATOA WITO KWA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA HII
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Benki ya kiislam imetoa wito kwa wananchi wa dini zote na wasio na dini kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopati...
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Benki ya kiislam imetoa wito kwa wananchi wa dini zote na wasio na dini kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana katika benki hiyo.
Benki ya kiislam
Wito huo umetolewa leo mjini hapa, na mkurugenzi wa huduma za benki ya kiislam, Said Mohamed Said, wakati wa semina ya siku moja iliyofanyika Katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Lindi.

Mohamed alisema benki hiyo ambayo hapa nchini ilianzishwa Januari 2011 huko Zanzibar, haibagui wateja kutokana na itikadi ya dini. Bali mtu yeyote anaweza kujiunga na kufaidika na fursa zinatotolewa na benki hiyo kupitia huduma zake. Ikiwamo mkopaji kukopa na kuweka bila riba.

Aliwaomba wananchi wapuuze dhana kuwa benki hiyo ipo kwa ajili ya waislam peke yao na ndio wenye haki ya kuwa wateja wake. Jambo ambalo halina ukweli wowote. Kwani hata katika nchi ambazo sio za kiislam na hazina waislamu wengi zinabenki za aina hiyo na zinatoa huduma kwa watu wadini nyingine na wasio na dini pia.

Mohamed alizitaja baadhi ya fursa ambazo wateja wa benki hiyo wanaweza kuzitumia na kufaidika nazo nipamoja na mkopo wa elimu na vifaa na zana mbalimbali ikiwamo vifaa vya ujenzi na zana za kilimo. Mikopo ambayo haitakuwa na riba kabisa. Kwani benki hiyo inafanya biashara kwa ushirikiano na wateja wake. Jambo ambalo nitofauti na benki nyingine ambazo msingi na muhimili wa uwepo wake ni riba.
"Benki yetu inakodisha vifaa na zana mbalimbali kwa utaratibu mzuri sana, vifaa na zana ambazo mwisho wa siku zinakuwa za mteja mwenyewe. Katika benki ya kiislam kuna biashara na faida, wakati katika benki zisizo za kiislamu kuna mikopo na riba, kwenye mkopo kunakuwa na riba lakini kwenye biashara kunakuwa na faida." alisema Mohamed.

Mkurugenzi huyo akitaja nafanikio ya benki tangu kuanzishwa kwake, alisema mwaka wakwanza walipofunga hesabu za mwaka walikuwa na amana za wateja zenye thamani ya jumla ya shilingi 5.00 bilioni. 

Hata hivyo hivi sasa inaamana za wateja zenye thamani ya takribani shilingi 120.00 bilioni. Lakini pia imeweza kuongeza idadi ya matawi yake kutoka tawi moja mwaka 2011 hadi sita mwaka huu.
"Mafanikio ni makubwa, benki inakuwa kwa kasi ya wastani wa 60% kwa mwaka, hata hivyo changamoto iliyopo ni uelewa mdogo wa mambo ya kitaaluma kwa wateja na watoa huduma. Kwasababu huduma zinazotolewa ni mpya na tofauti na benki nyingine," aliongeza kusema Mohamed.

Aidha Mohamed alisema katika kuhakikisha huduma zake zinapatikana kwa urahisi katika kanda hii ya kusini, benki hiyo inatarajia kufungua vituo vya kutolea huduma katika manispaa ya Lindi mkoani Lindi na mjini Masasi mkoa wa Mtwara. Kwa upande wake mwangalizi wa masuala ya kisheria wa benki hiyo, Ally Shariff, alisema tofauti nyingine baina ya benki hiyo na banki zisizo za kiislam ni kwamba benki hiyo inazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na muumba katika kutoa huduma zake. Wakati benki nyingine zinaendeshwa kwa mfumo wa sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na binadamu wenyewe.

Alisema benki hiyo haiangalii inapata nini katika kufanya biashara na wateja wake, bali jamii itanufaikaje na faida ya biashara itakayofanyika na aina ya biashara itayofanyika inamadhara na faida gani kwa jamii.
"Mambo hayaangaliwi kabisa kwenye mabenki mengine. Yenyewe yanaangalia yatanufaikaje, ukienda kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara ya pombe utakopeshwa bila kujali hiyo pombe inamadhara kwa watumiaji na jamii kwa jumla," alisema Shariff.

Semina hiyo iliyowashirikisha baadhi wananchi wa kawaida na wafanya biashara waliopo katika manispaa ya Lindi ilikuwa na lengo la kuwajengea uelewa kuhusu faida za kutumia benki hiyo.

********************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top