Unknown Unknown Author
Title: WILAYA YA NACHINGWEA KUTUMIA TSH 571.50 MILIONI KUTENGENEZA BARABARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. HALMASHAURI ya wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, imepanga kutumia Jumla ya Sh 571.50 milioni, kwa ajili ya m...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.HALMASHAURI ya wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, imepanga kutumia Jumla ya Sh 571.50 milioni, kwa ajili ya matengenezo kwa baadhi ya miundombinu ya barabara zenye urefu wa kilomita 41.88 na milimita 2,460 msimu ujao wa 2016/2017.
Ofisi ya DC wilaya ya Nachingwea
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bakari Mohamedi Bakari ameyaeleza hayo jana, alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii Ofisini kwake mjini Nachingwea.

Bakari amesema kazi za matengenezo hayo, zitafanyika muda wowote kufuatia Halmashauri hiyo, kupatiwa fedha kutoka Serikali kuu, zikiwemo Sh 22,409,280.27 zilizopindukia mwaka 2015/2016.

Amesema kati ya fedha hizo Sh 571.50 milioni zilizopatiwa na Serikali kuu, Sh 316.05 milioni zimetolewa na Mfuko wa maendeleo, ambazo zimepangiwa kufanya matengenezo maalumu kwa kiwango cha Lami barabara yenye urefu wa kilomita 2.70.

Mkurugenzi mtendaji huyo ametaja kazi zingine zitakazofanyika na gharama zake kuwa ni pamoja na matengenezo ya kawaida kilomita 31.98 kwa Sh,134.27 milioni, sehemu korofi kilomita 8.4 (Sh,152.19 milioni), ujenzi wa makalavati na mifereji milimita 2,460 itakayo ghalimu Sh 255.45 milioni.
“Kwa hivi sasa tupo katika hatua ya maandalizi ya kutafuta zabuni kwa ajili ya kutangaza kazi za matengenezo ya barabara kwa mwaka 2016/2017”Alisema Bakari.

Bakari amesema hali ya miundombinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo, hususani maeneo ya vijijini katika Halmashauri hiyo sio ya kuridhisha, kwani nyingi ni za udongo hivyo uharibika mara kwa mara kila zinapotengenezwa kutokana na maji ya mvua.

Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, ina mtandao wa barabara zenye Jumla ya urefu wa kilomita 701.7 kati ya hizo za wilaya zina urefu wa kilomita 327.8, za vijiji (Feeder-roads) km 333.7 na za mji mdogo wa wilaya hiyo zipo km 40.2.

*********************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top