MTANDAO WA WHATSAPP WAJA NA BORESHO HILI KATIKA TOLEO LAO JIPYA

Whatsapp
Katika toleo la Beta la simu za iOS, Mtandao wa Whatsapp wafanya boresho la Kumuwezesha mtumiaji kuwa na uwezo wa Kufuta ujumbe uliokwisha tumwa kwa Mtu mwingine.

Uwezo huo unaonekana katika eneo la "settings". Kikubwa ni kwamba utaweza kufanya hivyo kama tuu mtumiaji mwingine bado hajausoma ujumbe huo. Kama ukishasomwa basi hautaweza ufuta tena.

Jinsi inavyofanya kazi

Ukishatuma ujumbe basi utaweza kubofya na kuendelea kushikilia kwenye ujumbe huo ulioutuma na utapata mapendekezo mawili. ‘Edit’ yaana fanya maboresho au ufute "revoke". kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.

Hadi sasa WhatsApp wenyewe hawajatoa taarifa rasmi juu ya lini uwezo huo utakuja kwa watumiaji wote wa WhatsApp. Kikubwa ni kwamba ni kitu ambacho tukitegemee kuja katika toleo lolote jipya kwa sasa.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post