MEEK MILL NA NICKI MINAJI WAMEACHANA CHANZO KIKIWA NI USALITI KWA MWANAMKE HUYU HAPA

Taarifa zinasema Nicki Minaj na Meek Mill wameachana rasmi baada ya Meek Mill kumsaliti na mwanamke anayejulikana kama Sonye.
Nicki Minaj na Meek Mill
Jumalipi ya Dec. 18 mashabiki waligundua kuwa Meek na Nicki hawafatani tena kwenye mtandao wa Instagram na jambo hili limechochea taarifa za kutengana kwao.

Meek Mill aliweka picha Instagram iliyoambatana na ujumbe “$avage…just friends.” ila mpaka sasa haijajulikana mwanamke huyu ni nani…

Meek Mill na Nicki Minaj wamekuwa pamoja kwenye macho ya watu toka February 2015.

Bossip imeripoti kuwa Sonye ni mmiliki wa duka la nguo na amekuwa na Meek kwa zaidi ya mwka mmoja huku Meek akiwa na Nicki Minaj.

Pia Minaj na Meek Mill kwa sasa wanaishi nyumba tofauti huku kambi ya Nicki Minaj ikithibitisha kuwa hawako pamoja.
Sonye
Hii ndio post ya Meek Mill iliyoleta Drama
Meek Mill

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post