Unknown Unknown Author
Title: HALMASHAURI ZA LINDI NA MTWARA ZASHAURIWA KUTENGA BAJETI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Halmashauri mkoani Lindi na Mtwara zimeshauriwa kutenga bajeti kutokana na mapato ya mirahaba ya mafuta na gesi kwa ajili ya kuhamasisha m...
Halmashauri mkoani Lindi na Mtwara zimeshauriwa kutenga bajeti kutokana na mapato ya mirahaba ya mafuta na gesi kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu ili kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira.
Kituo cha GesiWito huo umetolewa leo na mratibu wa mradi wa kujenga uwezo kuhusu uziduaji, sera na sheria ya mazingira wa asasi ya kiraia ya jukwaa la utunzaji mazingira kanda ya kusini (SECOFO), Mustafa Kwiyunga, kwenye semina iliyofanyika leo katika Manispaa ya Lindi kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu.

Kwiyunga alisema madiwani wa halmashauri hawanabudi kutengeneza sheria ndogo zitazozifanya halmashauri zao zitenge fedha zinazotokana na mirabaha ya gesi na mafuta ili zitumike kuhamasisha jamii itumie nishati jadidifu ili kurekebisha athari za mazingira zinazoweza kutokea kutokana na uchimbaji wa gesi, mafuta na matumizi ya nishati nyingine zinazoweza kusababisha uharibifu wa mazingira. Ikiwamo ukataji wa misitu kwa matumizi ya kuni.
"Tunashauri mapato hayo yatengwe kwa ajili ya kusaidia matumizi ya nishati jadidifu, ikiwamo upepo na jua," alisema Kwiyunga.

Mratibu huyo aliongeza kusema kwakuwa lengo kubwa la mradi huo ni kupunguza athari za mazingira zinazotokana na uchimbaji wa gesi na mafuta.

Hivyo wananchi wanatakiwa kupata elimu itayowapa uwezo wa kutambua kwamba nishati jadidifu ni endelevu. Wakati nishati nyingine ikiwamo gesi na mafuta zitakwisha.

Aidha Kwiyunga alitoa kwa wachimbaji kuzingatia viwango vya kimataifa vya usalama wa mazingira. Akibainisha kwamba lengo ni kuhifadhi mazingira asilia. Ambapo wananchi wanahaki ya kuelewa gesi na mafuta yanapatikanaje, yanatumikaje na yanawafaidishaje.
"Ili wananchi waweze kuwa na maamuzi kwa rasilimali hizo, mapato yake yawekwe wazi na sehemu ya mapato hayo ipelekwe kwenye nishati jadidifu," alisema Kwiyunga.

Semina hiyo ya siku mbili iliyowashirikisha madiwani ambao
ni wajumbe wa kamati za uchumi na fedha wa halmashauri za wilaya za Lindi vijijini, Kilwa na manispaa za Lindi, maofisa mipango, maendeleo ya jamii na mazingira wa halmashauri hizo.


Pamoja na viongozi wa asasi za kiraia, iliandaliwa na jukwaa la mazingira la ukanda wa kusini (SECOFO), linalosimamiwa na mtandao wa mashirika yasio ya kiserikali ya mkoa wa Mtwara (MRENGO) kwa ufadhili wa mfuko wa shirika la uhifadhi wa mazingira duniani (WWF).
_________________________________________
  • ULIPITWA NA HII YA QEENDARLEEN KUMTOSA ALIKIBA?

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top