TANZIA: MBUNGE WA JIMBO LA DIMANI (CCM) AFARIKI DUNIA

Mhe. Hafidh Ali Tahir
Mhe. Hafidh Ali Tahir

Mhe. Spika anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani(CCM), Zanzibar.

Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya General hapa Dodoma.

Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae.

Mhe. Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.
**************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post