Unknown Unknown Author
Title: RAIS MAGUFULI APIGILIA MSUMARI MUSWAADA WA HUDUMA ZA HABARI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
“Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri sana kwa nchi hii, wale wanaoandika vizuri na hata wanaoongeza chumvi nawapenda wote. Mfano ndugu ...
“Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri sana kwa nchi hii, wale wanaoandika vizuri na hata wanaoongeza chumvi nawapenda wote. Mfano ndugu yangu kipanya anayenichora kwenye katuni saa zingine najitazama kwenye kioo kama nna kichwa kama vile anavyonichora … lakini yote kwa yote nipo pamoja nanyi na wala msiwe na wasiwasi i love you all”.
Rais Magufuli
Hayo ni maneno yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema leo alipokutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo tathimini ya utawala wake tangu akae madarakani ambapo kesho Novemba 5 anatimiza mwaka mmoja tangu kuapishwa kwake.


Alipoulizwa na Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) juu ya sheria zinazohusiana na tasnia ya habari kuwasilishwa bungeni kwa hati ya dhadhura kama ilivyokuwa kwa Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber Crime Act 2015), Sheria ya Takwimu na Sheria ya Muswaada wa Huduma za Vyombo vya Habari ambayo itataanza kujadiliwa hapo kesho huku wadau mbalimbali wakitaka kuongezewa muda ili wapate fursa ya kujadili kwa kina Rais Magufuli amesema wadau hao walipaswa kujadili mapema kwa kuwa tangu mwaka 2011 nafasi ya majadiliano ilikuwepo.
Tido Mhando
Akasisitiza kwa kusema “Tangu mwaka 2011 walipaswa kujiandaa kama miaka yote hiyo wameshindwa kufanya majadiliano hii miezi mitatu wanayoiomba ndio wataweza? Acha bunge lifanye kazi yake kwa kuwa tayari muswaada huo umekwisha wasilishwa na naomba nikuhakikishie sitakuwa mnafiki wakileta mezani kwangu nitasaini mara moja”.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top