MTIFUANO BADO UNAENDELEA..!! DIAMOND KUMBE ALIRUSHA JIWE GIZANI KUHUSU "PETE YA KIJANI" ALIKIBA KAJIBU MAPIGO

Najua utakuwa unaikumbuka kauli ya Diamond aliyoitoa wiki iliyopita kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM kuhusu pete ya kijani.
Alikiba na Diamond
Ngoja nikukumbushe japo kidogo kile alichokisema, “Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu.”

Kumbe alikuwa amerusha jiwe gizani kwa upande wa pili.
Alikiba
Inawezekana Alikiba king Kiba ameshtuka hilo kutokana na picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram na kuandika, “Pete Ya Kijani #BirthdayLoading29thNoV #KingKiba.”

Mwanzo ilionekana ilikuwa ni vita baridi ya maneno ya chini kwa chini kati ya mafahari hao lakini kwa sasa hakuna kilichojificha tena na kila kitu kipo wazi.

Wiki iliyopita hitmaker huyo wa Salome na Ommy Dimpoz walichafua hali ya hewa kwenye mtandao huo kwa kutupiana vita ya maneno ya kejeli na kukashifiana.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post