ZIARA YA KUSHTUKIZA YA RAIS MAGUFULI AIRPORT DAR ES SALAAM LEO

Leo October 5 2016 mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.
Rais Magufuli
Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa. 


Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.

"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua"

***************
TAZAMA JINSI PJ ALIVYOTAMBULISWA LEO CLOUDS FM

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post