Unknown Unknown Author
Title: WAZIRI MKUU AMUITA DODOMA MMILIKI WA KIWANDA CHA MAFUTA YA KULA ILULU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji am...
Waziri Mkuu Kassim
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji amekifanya kuwa Ghala nakukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa Kiwanda hicho kipo wilaya ya Rungwe Mkoani Lindi Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Rungwe Mkoani Lindi.
Waziri Mkuu Kassim
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyo haribika ambayo yalikuwa yanamilikiwa nakiwanda cha kukamua ufuta ILULU kiwanda hicho kipo wilani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliye kichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala lakuhifadhia bidhaa kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi. 
Picha na Chris Mfinanga

Na. Mwandishi Wetu, Nachingwea
Kutotumika kwa kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kula cha Ilulu kumesababisha waziri mkuu, Kassim Majaliwa amuite mmiliki wa kiwanda hicho kilichokuwa mali ya umma.

Majaliwa ametoa agizo hilo jana mjini Nachingwea alipokwenda kiwandani hapo ili kuona maendeleo ya kiwanda hicho baada ya kununuliwa muda mrefu.

Waziri mkuu baada ya kutoridhishwa na hali aliyoiona, amelazimika kumuita mmiliki huyo aende ofisini kwake tarehe 22 mwezi huu, saa nne asubuhi akiwa nanyaraka halisi za ununuzi aliofanya kutoka serikalini.

Majaliwa alisema serikali haiwezi kuwavumilia wawekazaji na wanunuzi wa mali ya umma wanaoshindwa kuendeleza na wanaobadilisha matumizi yaliyokusudiwa na serikali.

Alisema kutokana na wanunuzi na wawekezaji wengi kwenye miradi na mali za umma kushindwa kuiendeleza, kunahaja ya kufanya mapitio ya sheria ya uwekezaji ili kuona kama sheria zinaendana na lengo la ubinafsishaji.
"Maghala na viwanda kama hivi bora vingekuwa mikononi mwa halmashauri,ipo haja ya kupitia sheria za uwekezaji ili tuone kulitakiwa kufanyike nini,sheria inasemaje na wawekezaji walitakiwa wafanye nini," alisema Majaliwa.

Kiwanda hicho kabla ya kubinafsishwa kilikuwa kinatengeza mafuta ya kula yanayotokana na ufuta.Hata hivyo hakuna uzalishaji unaoendelea kiwandani hapo, majengo yake yamezungukwa na pori kukiwa hakuna dalili zozote za kiwanda hicho ambacho kinatajwa kilinunuliwa na marehemu Abass Gulamali, kuendelea na uzalishaji.
************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top