BAADA ya mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai kupiga marufuku mifugo kulishwa na kunyweshwa katika vijiji ambavyo havijawapokea wafugaji. Baadhi ya wafugaji waliangusha vilio mbele ya mkuu huyo wa wilaya huku wakimuomba awahurumie ili mifugo yao isife kwa kukosa maji.
Hayo yalitokea jana katika kijiji cha Somanga Kusini wakati wa kikao cha wafugaji na mkuu huyo wawilaya ambae alikwenda kukutananao ili kusisitiza agizo lake la kuwataka wakulima waliovamia maeneo yaliyotengwa kwa ufugaji wahame, na wafugaji waache kwenda kulisha kwenye maeneo na vijiji ambavyo sio miongoni mwa vijiji 22 vilivyokubali kuwapokea na kuishi nao.
Wafugaji hao walisema agizo hilo litasababisha mifugo yao kufa kwakosa maji. Kwasababu lambo walilokuwa wanatumia kunyweshea limekauka. Hivyo wanalazimika kwenda kunywesha vijiji ambavyo sio miongoni mwa vijiji vilivyoridhia kuwapokea.
Ikiwamo kijiji cha Kinjumbi ambacho wananchi wake wanalalamika kuvamiwa na makundi ya ng'ombe nakuharibu mazao ya kilimo.
Wafugaji hao licha ya kutakakujua watanywesha wapi mifugaji yao badala ya Kinjumbi, walisema sababu ya kukauka lambo walilokuwa wanatumia ni wakulima kuvamia na kuendesha shuguli za kilimo kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ufagaji.
Mzee Kazamoyo Makwaya, huku akidondosha machozi alisema serikali imeamua kuwafilisi ili wawe masikini. Kwamadai kwamba mambo mengi waliyohaidiwa na serikali wakati wanahama kutoka Ihefu kuja mikoa ya kusini kwakiasi kikubwa hayatekelezwa.
"Tuliahadiwa majosho, shule, marambo, madawa na maeneo ya kufugia, lakini tangu nimekuja ninamiaka tisa hakuna yaliyofanyika zaidi ya lambo ambalo linamefukiwa na wakulima," alisema mzee Kazamoyo.
Mzee huyo(70) alisema hawapeleki mifugo katika vijiji hivyo kwa kiburi lakini hawana njia ya kuokoa mifugo yao kufa.
Nganga Mbeho, alisema wanaishi na kunyanyaswa kama sio raia halali. Kwamadai kuwa eneo lilotengwa limevamiwa nawakulima, mifugo hata inapokula mabua makavu ya mazao yaliyovunwa wanaadhibiwa.
Alisema mwaka huu pekee wamelazimika kulipa takribani 27.00 milioni kama faini. Huku kesi nyingi zinaendelea mahakamani.
Mfugaji mwingine, Donalt Mbaga, alisema sababu ya migogoro baina yao nawakulima nikutoheshimiwa mipaka na maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Mfugaji huyo alisema iwapo wataheshimu mipaka na maeneo hayo itakwisha tupotayari kushirikiana na serikali, hata lile lambo tupotayari kufukua ikiwa serikali itatia nguvu pia.
Lakini kwa sasa mifugo tutanywesha wapi, maana tukiheshimu agizo tunahalalisha mifugo yetu ife kwa kiu," alisema Mbaga huku akimwaga machozi.
Akijibu hoja, malalamiko na maombi ya wafugaji hao, Ngubiagai alisema chanzo cha migogoro mingi ni baadhi ya viongozi, watendaji na wananchi kushindwa kutii, kusimamia na wengine wanapindisha sheria kwa masilahi yao binafsi.
Hivyo yeye hapendi na hatarajii kuwa nimiongoni mwa wasiotii sheria na wanaosababisha migogoro badala ya kutatua.
Aliwataka wafugaji hao kushirikiana na serikali katika kushugulikia changamoto walizonazo kwenye eneo walilopewa, badala yakupeleka mifugo maeneo na vijiji yasivyo husika.
"Ofisa mifugo tafadhali waoneshe haraka maeneo yanayopatikana maji katika vijiji 22 vilivyokubali kuwapokea waende wakati tushugulikia changamoto hizo," alisema Ngubiagai.
Mkuu wa wilaya alisisitiza wakulima waliovamia maeneo yaufugaji waondoke ndani ya wiki mbili. Nawafugaji waache kupeleka mifugo katika maeneo yasiyositahili.
Wilaya Kilwa hadi sasa ina upungufu wa ngombe 56437 wanaoweza kujaza maeneo yaliyotengwa kwa ufugaji. Kwasababu hadi sasa inadadi ya ng'ombe 27279 tu, wakati mahitaji halisi ni ng'ombe 83427.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.