PAUL JAMES ‘PJ’ AREJEA CLOUDS FM NA KUTAMBULISHWA KWENYE XXL TAZAMA VIDEO

Paul James ‘PJ’ amerejea tena Clouds FM akitokea EFM. Anakuwa mtangazaji wa pili wa EFM kuchukuliwa na Clouds katika kipindi cha mwezi mmoja, baada ya Kicheko.
Clouds FM
PJ aliyeondoka Clouds mwanzoni mwa mwaka huu akiwa na Gerald Hando, ametambulishwa rasmi Jumatano hii. Anamfuata mtangazaji mwingine aliyehama Clouds akaenda EFM na kisha kurejea tena kwenye kituo hicho, Gardiner G Habash.

Mtangazaji huyo anayesifika kwa uhodari wa kuchambua magazeti, alikuwa na mchango mkubwa wa kukifanya kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM kujipatia umaarufu ndani ya muda mfupi. 


Je? Kupokonywa kwa PJ EFM kunachocheza zaidi uhasama kati yake na Clouds FM. Hebu tupe maoni yako hapo chini.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post