Unknown Unknown Author
Title: SERIKALI YAONGEZA MUDA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Serikali imeongeza muda wa usajili wa vitambulisho vya taifa kwa watumishi wa umma, na kutoa onyo kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya umm...
Serikali imeongeza muda wa usajili wa vitambulisho vya taifa kwa watumishi wa umma, na kutoa onyo kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya umma watakaoshindwa kusimamia zoezi hilo.
Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba.

Uamuzi huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba, kwa pamoja na Waziri wa Nchi Utumishi na Utawala Bora Angela Kairuki wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Waziri Nchemba amesema kuwa watumishi waliokosa baadhi ya nyaraka wamepewa muda wa siku 14 kukamilisha utaratibu wa kutafuta nyaraka hizo ili kufanikisha zoezi hilo huku akisema kuongeza muda huko kunatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu huo wa baadhi ya nyaraka.

Kwa upande wake Mhe. Angela Kairuki ametoa onyo kwa viongozi watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo ambalo limepangwa kufanyika kwa nchi nzima.
***********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top