Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Patricia Kisoti Muuguzi anayetuhumiwa kufanya uzembe uliosababisha Mama mjamzito kujifungua na mtoto wake kupoteza maisha katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Baadhi ya watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya katika Mkutano na Mkuu wa Wilya y chunya mara baada ya kutokea tukio la mama mjamzito aliyepoteza mtoto wakati akijifungua kutokana na uzembe wa mmoja wa wauguzi hospitalini hapo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kufanyiwa ukatili kwa mama mjamzito na mmoja wa wauguzi.
Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Na Mwaandishi Wetu, Mbeya
Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi wa afya katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito kujifungua mtoto akiwa amekufa.
Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama na kimetia aibu sekta ya afya.
Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, mjamzito huyo akiwa ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku, wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.
Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na kushindwa msaada wowote.
Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.
Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.
Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.
Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema siku hiyo, yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake, walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa umefungwa.
Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mateso hayo mpaka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa oparesheni.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni, ndani yake kulikuwa na uzembe.
**************
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.