Unknown Unknown Author
Title: MZEE AKILIMALI - "YANGA HAIWEZI KUKODISHWA KAMA MASUFURIA YA KWENDA KWENYE SHUGHULI"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Siku kadhaa kabla ya kufanyika mkutano wa Yanga, Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa Yanga imezungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo amb...
Mzee akilimali
Siku kadhaa kabla ya kufanyika mkutano wa Yanga, Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa Yanga imezungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo ambao mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji anataka autumie katika kuingia mkataba wa miaka 10 kuimiliki nembo ya klabu.

Katibu wa Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimalia amesema ambacho Manji anakifanya kinaweza kusababisha timu hiy ikaingia katika vurugu ambazo hazikuwepo kwa muda mrefu kwa sababu njia ambayo anatumia inawagawa wanachama na mashabiki kwa wengine kuutaka mfumo na wengine kuukataa.

“Hatutaki kurudi kule tulipokuwepo katika mgogoro wa miaka saba, mwaka 2003 ndiyo tukapata usuluhisho na kukubaliana kuwa litumike jina ambalo lilikubaliwa na waasisi wetu, tukakubaliana kuwa kuwe na Yanga SC na Yanga Cooperation,

“Yanga kampuni ilifishwa na kukawa na utaratibu kuwa kuwe na hisa, Yanga SC kuwe na hisa 51 na wanachama wawe na asilimia 49, na tulizunguka mikoa mingi ili kufuta mgogoro uliokuwepo na kuomba ridhaa ya wanachama wa klabu kukubali hisa,” alisema Akilimali na kuongeza.

“Tulipata mwenyekiti mpaka anatoka timu ilikuwa na Mil. 200, tukampata bwana Nchunga yeye akajiuzulu baada ya miaka miwili, tukamchagua Bwana Manji akaongoza kwa miaka miwili, kwasababu tu ya upenzi ikabidi tuikanyage katiba akaongeza muda, ili tujipange na yeye ajipange ili tutafute kiongozi wa baada yake, na tukafikia hatua ya kumchagua kwa mara nyingine,

“Haijafika hata miezi nane imeibuka swala la deni la Bilioni 11 na laki sita, jambo ambalo limetushtusha sana wanayanga, limekuja tamko la mwenyekiti kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na lebo yake kwa muda wa miaka 10, kwasisi wote tunasema Yanga ni kubwa sana, Yanga haiwezi kukodishwa kama masufuria ya kwenda shughulini. Kupitia mimi na wazee wa kamati tumesema hatukubaliani na hilo”

Nae aliyekuwa Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga, Mohammed Msumi amesema kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na klabu ni vyema akakaa pembeni na kuanzisha timu yake mwenyewe na kuacha Yanga iendeshwe na mfumo ambao umezoeleka.

“Kwanini anataka hili jambo haraka haraka na wakati alisema Yanga inajiendesha kwa hasara, mfanyaniashara gani anakaa sehemu ya aina hiyo, kama hawezi kufata utaratbu anaweza kuanzisha timu nyingine sio kuitaka yanga na kutumia mamlaka kwa mabavu ili tu aipate Yanga,” alisema Msumi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top