HUDDAH SIO MTU WA MCHEZO MCHEZO AMNYEMELEA RAYVANNY, AMWANDIKIA UJUMBE HUU HAPA

Kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa ameshawahi kutoka kimapenzi na Hit maker wa Single ya "Aiyola" Harmonize (japo wenyewe walikanusha) kutoka katika label ya WCB, Sasa Mlimbwende kutoka Kenya Huddah amnyatia Rayvanny hit maker wa Single ya "Kwetu" na "Natafuta Kiki" pia Kutoka Label ya WCB.
Huddah
Ubuyu huo umekuja baada ya Rayvanny kupost Picha katika Mtandao wa Instagram na Kuandika ujumbe uliosomeka "Unahisi nini kimenifanya nizubae".


Katika hali isiyotarajiwa akatokea mlimbwendehuyo na kujibu Swali hilo kwa kuandika "Ukipata hela nyingi utakuwa mzuri sana..... I'll be waiting". Kufuatia ujumbe huo uliowatoa watu povu kupitia post hiyo kwa kusema mlimbwende huyo anamtaka kimapenzi msanii huyo.
Rayvanny
Lakini Rayvanny hakuiacha ipite kimya kimya naye alijibu mashambulizi kwa kusema kuwa "Hahahahahah Zipo nyiiiiiiingi ushindwe wewe tu" huku akimtag Huddah.
post
Je nini maoni yako juu ya Couple hii.
***************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post