BABU TALE AIKACHA SHEREHE YA NDOA YA MSANII TUNDA MAN

Siku ya Jana msanii Captain Tundaman kutoka Tiptop Connection iliyopo chini ya meneja Babu Tale amefanikiwa kutimiza nusu ya dini kwa imani ya dini yake (Kufunga ndoa) huko mjini Morogoro.
Ndoa ya Tunda Man
Kitu ambacho ni cha kustaajabisha na kilichozua mjadala katika siku hii muhimu kwa msanii Tundaman ni kwamba meneja wake Babu Tale hakuweza kuhudhuria katika tukio hilo muhimu la msanii wake. Ukizingatia timu nzima ya wasanii wa Tiptop Connection walikuwepo eneo la tukio.

Kitu ambacho kimewashangaza wengi na kuzua maswali kibao ya sintofahamu huku wakijadili kuwa endapo ingekuwa ni shughuli ya msanii Diamond Platnumz (ambaye ni anammeneji pia) je! meneja huyo angeshindwa kuhudhuria?
Ndoa ya Tunda Man
Lindiyetu.com imeona nivyema kufikisha madukuduku ya wadau, wewe kama mpenzi na mmoja wa wafuatiliaji wa tasnia ya burudani una kipi cha kusema juu ya hili? 

Tu-shee mawazo hapa chini kwenye uwanja wa comments.
****************

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post