MRISHO NGASSA AVUNJA MKATABA NA FREE STATE, JE ANATAKA KUJIUNGA NA TIMU GANI? SOMA HAPA KUJUA

Winga Mrisho Ngassa amevunja mkataba na timu ya Free State Stars ya Afrika kusini baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano.
Mrisho Ngassa
Ngassa alijiunga na klabu hiyo Mei 2015 ambapo alisajiliwa na kocha Kinnar Phiri na kudondosha wino wa miaka minne kwa sasa mchezaji huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote.

Klabu ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini ilitoa barua ya kuvunjwa mkataba huo na Meneja Mkuu Rantsi Mokena inaonesha mkataba huo umevunjwa tangu August 25, 2016.
Barua ya Ngasa
Kupitia akaunt yake ya instagram, Ngasa ame-post picha inayoonesha akiwa katika timu mbalimbali ambayo imeambatana na ujumbe.
instagram, Ngasa

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post