NIJUZE NIJUZE Author
Title: KARIAKOO FC YAICHAPA ABAJALO FC 1-0
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Wachezaji wa Kariakoo Wakishangilia Kwa Pamoja baada ya kufunga Goli pekee lilioipa ushindi Timu hiyo katika Mchezo baina yao na Abajalo Fc...
DSC05012Wachezaji wa Kariakoo Wakishangilia Kwa Pamoja baada ya kufunga Goli pekee lilioipa ushindi Timu hiyo katika Mchezo baina yao na Abajalo Fc.DSC05008Kocha wa Abajalo Dell Pielo akizomewa na washabiki wa Kariakoo Fc, Ikumbukwe kocha huyu ndio yule alieifikisha Timu ya Miundombinu kufika Fainali lakini inasemekana kuwa aliuza mechi hiyo na kushindwa kuchukua Kombe.DSC05007 
Wachezaji wa Abajalo Fc wakitoka katika Chumba cha kupumzikia ndani ya Uwanja wa Ilulu. (Kariakoo Fc 1 – Abajaro 0).
Na: Fungwa K, Lindi
Timu ya Karikoo Fc ya mjini lindi leo imeshuka dimbani kumenyana na timu ya Abajalo Fc ya mjin Dar es salaam.
Kipute hicho kilipigwa katika dimba la ILULU ikiwa uwanja huo ukiwa na historia ya kutoiruhusu timu ngeni kuondoka na ushindi.
Mpira ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa kasi, kadri muda ulivyokuwa ukisogea Abajalo Fc walionekana kuutawala mchezo huo kwa kuweza kufika langon mwa Kariakoo Fc mara nyingi lakin ngome ya Kariakoo FC ilikuwa imara, hada mapumziko timu zilitoka suluhu.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya kariakoo kuliandama lango la Abajalo na kuweza kupata penalt, kaptain wa kariakoo alishindwa kuiwezesha timu yake kuongoza kwan alipiga penalt hiyo na mpira kwenda nje.
Ni muksin ndiye alie wainua mashabiki mara baada ya kufunga goli maridadi kwa kupokea mpira wa cross uliopigwa na salum abdalah naye kupiga kichwa maridadi na kutinga wavuni.
Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalibakia

KARIAKOO LINDI 1-0 ABAJALO FC.
Agg 3-2., hivyo Kariakoo inasonga mbele katika hatua ya 3, ambapo itacheza na mshindi wa kesho kati ya FRANCE RANGERS (Dar) au AFRICAN SPORTS (Tanga)
DSC05004Mashabiki walifurika Ndani ya Uwanja wa Ilulu Kushuhudia mtanange kati ya Kariakoo Fc na Abajalo Fc kutoka Sinza Dar es Salaam. ( Kariakoo Fc 1 – 0 Abajalo Fc)DSC05014Wachezaji wa Akiba wa Timu wa Abajalo wakifuatilia kwa makini Mechi hiyo iliyokwenda kwa timu hiyo kufungwa goli moja bila.DSC05013
DSC05011Wachezaji wa Abajalo Fc wakimzonga Refa mara baada ya kuamulu Penalt kwa upande wa Kariakoo Fc, lakini Kariakoo Fc walikosa Penalti hiyo.

About Author

Advertisement

 
Top