Na. Ahmed Abdallah, Kilwa Masoko.
KATIKA kukabiliana na vitendo viovu katika pwani ya wilaya ya Kilwa katika bahari ya Hindi.
Mkuu wa wilaya hiyo,Christopher Ngubiagai ameagiza makambi yote ya uvuvi yafungwe hadi pale yatakapo hakikiwa na kukaguliwa.
Ngubiagai alitoa agizo hilo, juzi katika kijiji cha Kilwa Kisiwani alipokuwa anazungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
Alisama uwepo makambi mengi ya uvuvi ambayo hayajulikani idadi yake na wamiliki kunachingia vitendo viovu ambavyo havikubaliki kwa mujibu wa sheria.
Ngubiagai alisema baadhi ya makambi hayo ambayo ambayo yanafahamika kwa jina la madago, baadhi yake yanatumika kupitisha na kuhifadhi Madawa ya kulevya, kupitisha wahamiaji haramu, bidhaa za magendo na kusafirisha kutoroshea mazao ya misitu.
"Hata biashara ya ukahaba zinafanyikia humo, mbao, mkaa na maliasili nyingine zinapitishiwa na kuhifadhiwa humo," alisema Ngubiagai.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ambae anamuda mfupi tu tangu ahamie katika wilaya hii, amesema makambi hayo yafungwe hadi pale yatakapo kaguliwa na kuhakikiwa ili kuwajua wamiliki na wanaoishi kwenye kambi hizo.
Aidha aliwaomba wananchi wilayani humo kushirikiana na serikali katika kutoa taarifa kuhusiana na vitendo viovu na wanaotenda vitendo hivyo.
"Kila raia ni mlinzi katika nchi hii, toeni taarifa kuhusiana na vitendo vya kihalifu, bidhaa zinapoingia au kutolewa bila kulipiwa ushuru ni uovu ambao hata nyinyi wananchi mnaathirika nao maana fedha hizo ambazo zingelipwa kama ushuru zingetumika kuboresha huduma za jamii".
Ngubiagai yupo katika ziara ya kikazi ili kuhimiza shuguli za maendeleo katika vijiji vya wilaya humo.
Hadi sasa ameshatembelea na kuzungumza na wananchi katika vijiji vya Matandu, Milumba, Mavuji, Mandawa na Kilwa Kisiwani.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.