Ndg: Odilo Majengo Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wizara ya Viwanda na Uwekezaji Akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la wizara hiyo lililopo Viwanja vya Nane nane Ngongo Mkoani Lindi, Odilo amewataka wananchi kwa ujumla kutembelea Banda hilo iliwaweze kujionea na kufahamu uhusiano wa Kilimo na azma ya Tanzania ya Viwanda kama kaulimbiu ya Serikali ya awamu ya Tano inavyoeleza. Aidha amewataka wakulima kuuza mazao yaliyosindikwa ilikuweza kupanua masoko.
Ndg: Edwin N Rutageruka mkurugenzi wa Tantrade Tanzania Akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la wizara hiyo lililopo Viwanja vya Nane nane Ngongo Mkoani Lindi, Aidha Rutageruka ameeleza kuwa moja ya shabaha ya wizara ni kuwaunganisha wazalishaji na wanunuzi ilikufanikisha bidhaa hiyo kuuzwa katika soko la ndani na nje kwa ujumla. pia amewataka watanzania kupenda kununua bidhaa za ndani kuliko kutegemea sana bidhaa zinazotoka nje ili kukuza uchumi na kuongeza kipato cha wakulima nchini.
Moja ya Zana za Kilimo zilizo Buniwa na kiwanda cha Sido Lindi.
Moja ya Zana za Kilimo zilizo Buniwa na kiwanda cha Sido Lindi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.