Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WAOMBWA KUOKOA MITI ILIYOHATARINI KUTOWEKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Wananchi wametakiwa kutumia miti laini badala ya migumu kwa matumizi mbalimbali ilikuokoa miti migumu ambayo sasa ip...
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Wananchi wametakiwa kutumia miti laini badala ya migumu kwa matumizi mbalimbali ilikuokoa miti migumu ambayo sasa ipo hatarini kutokana na mahitaji na matumizi makubwa kuliko idadi ya miti hiyo.
miti kutoweka
Wito huo umetolewa leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi na Mkuu wa Idara ya ujenzi wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Oswin Komba alipozungumza na wananchi waliotembelea banda la maonyesho ya mamlaka hiyo. 

Komba alisema wananchi wanatakiwa kubadilika nakuacha kuamini kuwa miti migumu pekee inafaa kwa kutengeneza samani, badala yake watumie miti laini ambayo inachukua muda mfupi kukua tofauti na miti migumu ambayo ni michache na inachukua muda mrefu kukua hadi kukomaana kufaa kutumika. Alibainisha miti migumu ipo hatarini kutoweka na kusababisha vizazi vijavyo kushindwa kuikuta.

Sambamba na wito huo, Komba aliwaasa wananchi kuthamini bidhaa zinazotengenezwa nchini badala ya nje, kwani zina ubora wa hali ya juu.
"Uzalendo ni pamoja na kuthamini bidhaa tunazotengeneza wenyewe, wakati serikali inasisitiza uchumi wa viwanda ni muhimu wananchi wajenge tabia ya kuthamini bidhaa zetu," alisema Komba.

Baadhi ya wananchi licha ya kuishukuru serikali kuteua mkoa wa Lindi kufanyika maonyesho ya Nane Nane waliipongeza kwa kuanzisha mamlaka hiyo ambayo imekuwa ni mkombozi wa vijana katika kupata ajira baada ya kupata ujuzi kutoka VETA. 

Omari Rashidi, Mkazi wa kijiji cha Rutamba alisema VETA imekuwa mkombozi kwa vijana wanaomaliza masomo katika shule za msingi na sekondari ambao hawakubahatika kuendelea na elimu ya juu.
"VETA kila mwaka wanatuonesha mazuri, na wengi wetu tumenufaika na teknolojia yao katika shughuli za kilimo na uvuvi,".

Mwananchi huyo alibainisha kuwa wananchi wengi wamenunua pampu za maji ambazo zinatumika kumwagilia maji na dawa Mazao ya Kilimo kwenye Bustani zao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top