Vipengele vya tuzo mpya zilizoanzishwa na kituo cha runinga cha East Africa Televisheni, EATV Awards, vimetangazwa Ijumaa hii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mkuu wa masoko wa kituo EATV, Roy Mbowe alisema tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.
Vipengele hivyo ni:

- Mwanamuziki bora wa kiume
- Mwanamuziki bora wa kike
- Mwanamuziki bora chipukizi
- Kundi bora la muziki
- Video bora ya muziki
- Wimbo bora wa mwaka
- Muigizaji bora wa kiume
- Muigizaji bora wa kike
- Filamu bora ya mwaka
- Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.
Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanaotaka kushiriki watalazimika kujaza fomu za kutaka kutajwa kwenye tuzo na kuwasilisha kazi husika ambapo mchakato wa uchambuzi wa kazi hizo utachukua kipindi cha mwezi mmoja kabla ya majina yaliyoingia kwenye tuzo hizo kutajwa na kuanza kupigiwa kura.
Hata hivyo amedai kuwa pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi.
Hata hivyo amedai kuwa pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi.
Hata hivyo kumekuwa na maoni tofauti ya wadau ya kukosoa vipengele hivyo kwani wengi wamelalamikia kukosekana kwa vipengele muhimu katika tasnia hiyo ya Muziki na Filamu, Vipengele ambavyo vimesemwa kusahaulika na waandaaji wa Tuzo hizo ni:
- Wimbo Bora wa Hip hop
- Msanii Bora wa Hip Hop
- Mtayarishaji Bora wa Mwaka (Muziki na Filamu)
- Muongozaji Bora wa Mwaka ( Muziki kwa Video za wasanii na Filamu).
Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tags
HABARI ZA KITAIFA