Akiripoti kuhusu tukio hilo kwenye kipindi cha Papaso cha TBC, Baghdad amesema kuwa chanzo cha kifo cha marehemu bado hakijawekwa hadharani lakini taarifa za mwanzo zinaeleza kuwa msanii huyo alifikwa na mauti yeye na rafiki yake wakiwa katika tukio linalosadikiwa kuwa ni la kijambazi na inaelezwa kuwa marehemu na wenzake wamekuwa wakijihusisha na matukio hayo mara kwa mara kwa kivuli cha heshima waliyo nayo kwenye jamii.
Marehemu Ude Ude na rafiki yake Iku ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo enzi za uhai wao
Marehemu Ude Ude alijipatia umaarufu kwenye muziki wa bongo fleva kwa umahiri wake wa kuwatungia nyimbo wasanii ambapo nyimbo alizozitunga ni pamoja na Wangu na Yahaya za Lady Jay dee. Wimbo wake ulioweza ku hit ni Ngoma Inogile waweza icheki hapo chini.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.