NIJUZE NIJUZE Author
Title: LINDI SEKONDARI YAPOKEA MSAADA WA VITI NA MEZA 25 NA MILIONI 1 KUTOKA KWA WANAFUNZI WALIOSOMA MWAKA 1985-1988
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Katika Kuhakikisha Shule ya Lindi Sekondari ya Mkoani Lindi inarudi katika hali yake ya kawaida mara baada ya kukumbwa na tukio la kuungua ...
Katika Kuhakikisha Shule ya Lindi Sekondari ya Mkoani Lindi inarudi katika hali yake ya kawaida mara baada ya kukumbwa na tukio la kuungua moto na kusababisha hasara kubwa, leo hii Kikundi cha wanafunzi waliosoma katika shule hiyo kwa mwaka 1985-1988 wameweza kutoa Msaada wa Viti na Meza 25 kwa ajili ya kupunguza uhaba wa Meza na Viti ulioikumba shule hiyo baada ya janga hilo la moto lililotokea Hivi karibuni.
Msaada Lindi Sec School
Mkuu wa Shule Lindi Sekondari Honorat Tarimo akipokea Msaada wa Viti na Meza na kiasi cha Tsh Milioni 1 kutoka kwa Mhasibu wa Kikundi cha Wanafunzi waliosoma Shule hiyo Mwaka 1985-1988, leo hii tarehe 6/8/2016.

Wanakikundi hao licha ya Kutoa msaada huo wa Samani pia wameshatoa Pesa tasilimu kiasi cha Tsh milioni Mbili hadi hivi leo.

Wakikabidhi msaada huo kwa Mwalimu mkuu wa Shule ndg. Honorat Tarimo mbele ya baadhi ya wanafunzi na waalimu wa shule hiyo wamewataka wanafunzi kuvitunza vifaa hivyo kwani kufanya hivyo kutawatia moyo watu wengine kujitolea kuichangia shule hiyo ambayo kwa sasa inahitaji Samani nyingi hasa Viti na Meza.
Msaada Lindi Sec School
Mkuu wa Shule Lindi Sekondari Honorat Tarimo (katikati) akipokea Msaada wa Viti na Meza kutoka kwa Ndg Alfred Benno Magan ambaye ni kiongozi wa kikundi cha wanafunzi waliosoma Shule hiyo mwaka 1985-1988, leo hii tarehe 6/8/2016.

Honorat Tarimo Akiwashukuru kikundi hicho amesema kuwa Shule inawashukuru kwa msaada ambao wameutoa na pia amewaomba watu wengine kuiga mfano huo ili kuinusuru shule hiyo na upungufu huo uliopo.

Shule hiyo iliweza kupoteza Viti na Meza 360 ambavyo viliungua na hadi sasa wameweza kupokea Viti na Meza 109 hadi tarehe ya leo hivyo kufanya Shule hiyo kuwa na Upungufu wa Viti na Meza 251.
Msaada Lindi Sec School
Walimu wa Shule ya Lindi Sekondari wakishuhudia makabidhiano ya Msaada wa Viti na Meza na kiasi cha Tsh Milioni 1 kutoka kwa kikundi cha wanafunzi waliosoma shule hiyo Mwaka 1985-1988, leo hii tarehe 6/8/2016.

Honorat Tarimo Amewaomba wadau kuendelea kujitokeza kuisaidia shule hiyo ili kumaliza tatizo lililopo.

Msaada Lindi Sec School
Wanafunzi wa Shule ya Lindi Sekondari wakishusha Viti na Meza ambavyo vimetolewa kama msaada kutoka kwa kikundi cha Wanafunzi waliosoma Shule hiyo Mwaka 1985-1988, leo hii tarehe 6/8/2016.
Msaada Lindi Sec School
Moja ya wanafunzi waliosoma Shule ya Lindi Sekondari ambao ni wanakikundi cha Wanafunzi waliosoma Shule hiyo Mwaka 1985-1988.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top