NIJUZE NIJUZE Author
Title: RPC CUP - LINDI :: KITUMBI KWELA HOI KWA MITANDI, MAKONDE YAIADHIBU MIKUMBI 5 - 0.
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Ndani ya Uwanja wa Ilulu leo hii Ligi ya RPC Mkoa wa Lindi imeendelea kwa kuzikutanisha Timu nne kutoka katika makundi mawili, Kundi A Ka...
Kitumbikwela Vs Mitandi
Ndani ya Uwanja wa Ilulu leo hii Ligi ya RPC Mkoa wa Lindi imeendelea kwa kuzikutanisha Timu nne kutoka katika makundi mawili, Kundi A Kata ya Kitumbikwela walikuwa wenyeji wa Mitandi huku Kundi B ikizikutanisha timu za Kata za Makonde na Mikumbi.

Mechi ya Kwanza ilikuwa kati ya Kitumbikwela dhidi ya Mitandi ambayo mechi hiyo ilichezwa mnamo saa Nane mchana kama ilivyo ada.
Mitandi
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Mitandi kilichocheza dhidi ya timu ya Kitumbikwela.

Katika mechi hiyo Kitumbikwela walikubali kipigo cha Bao 5 - 1. Mitandi haikuwa na Kazi kubwa sana katika mchezo wa leo kwani ilionekana wamejiandaa vilivyo kwani iliwatumia dakika 2 tu kuzifumania nyavu za wapinzani wao kupitia  mchezaji wao Hassan Said. 

Dakika 14 baadae ni Maulidi Manyanya aliipatia timu yake ya Mitandi bao la pili.

Richard Edgar aliweza kuifungia goli la Kufutia machozi timu yake ya Kitumbikwela mnamo dakika ya 26. Hadi kipindi cha Kwanza kinamalizika Matokeo yalikuwa 2-1.
Kitumbikwela
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Mitandi kilichocheza dhidi ya timu ya Kitumbikwela.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kufanya mabadiliko kwa timu zote mbili lakini bado timu ya Kitumbikwela ilionekana kuzidiwa na dakika ya 51 Hassani saidi aliweza kuifungia goli la 3 timu yake hiyo, Dakika ya 64 Peter jololo alifunga goli la 4 huku goli la tano na la Ushindi liifungwa na Hassani Saidi tena na kuweza Kufunga Hattrick ya Kwanza katika Michuano hiyo.

Hadi Kipyenga cha mwisho matokeo yalisoeka Kitumbikwela 1 - Mitanda 5

Makonde Vs Mikumbi
Timu zikiingia Uwanjani: Kata ya Makonde dhidi ya Mikumbi.

Mnamo Saa Kumi za Jioni Timu ya Kata ya Makonde iliweza kuiadhibu timu ya Kata ya Mikumbi kwa kuifunga magoli 5 - 0 japo Mikumbi waliweza kupata nafasi ya Penalt na kushindwa kuitumia. 

Magoli ya Makonde yalifungwa na Juma Kado (dak 10, 33, 69), Mohamed Hamis (dak 24 Penalt), Muksin Rashid (dak 52), 
Makonde Vs Mikumbi
Timu zikisalimiana Kabla ya Mchezo kati ya Makonde dhidi ya Mikumbi.
Makonde Vs Mikumbi
Kesho mashindano hayo yataendelea kwa Kuzikutanisha Timu ya Maafisa wa Polisi Vs Kata ya Matopeni.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top