NIJUZE NIJUZE Author
Title: PROFESSOR JAY ACHANGANYA HIP HOP NA KISINGELI, AMSHIRIKISHA SHOLO MWAMBA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mikumi, Professor Jay ameingia location wiki hii kushoot video ya wimbo wake mpya aliyomshirikis...
Msanii wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mikumi, Professor Jay ameingia location wiki hii kushoot video ya wimbo wake mpya aliyomshirikisha msanii wa muziki wa kisingeli, ‘Sholo Mwamba’.
Professor Jay
Professor akishuka uwanja wa fisi kwa ajili ya kuanza kushoot video hiyo
Rapper huyo ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop kuchanganya ladha ya muziki wa Hip Hip na Kisingeli amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya kazi hiyo.

Kupitia instagram, Professor Jay ameandika:
Kazi kazi video shooting. Kwa heshima kubwa sana tumeshoot video hii maeneo ya Manzese – Uwanja wa Fisi Tukiwapa tumaini jipya na nguvu wale wote waliokata tamaa na kuwaambia wakomae kwa kufanya kazi ipo siku mambo yatakuwa sawa. Kazi kazi . Professor Jay Featuring Sholo Mwamba.
Wimbo huo umeandaliwa na mtayarishaji Mesen Selekta na video imeongozwa na mtayarishaji wa video anayekuja kwa kasi, Travellah

Angalia picha za maandalizi ya video hiyo.
Professor Jay
Professor Jay
Professor Jay

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top