Unknown Unknown Author
Title: NSSF YACHANGIA MILIONI 50 HARAMBEE YA UJENZI MPYA WA LINDI SEKONDARI, AHADI YAFIKA TSH MILIONI 640
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiongozwa na Meneja wa Mkoa wakiwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi Kwa Ajili ya Harambee Hiyo Il...
NSSF-Harambee Lindi
Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiongozwa na Meneja wa Mkoa wakiwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi Kwa Ajili ya Harambee Hiyo Iliyoendeshwa na Waziri Mkuu.

Na. Abdulaziz Video, Lindi
Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF Makao Makuu ikishirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Lindi Imechanga Jumla ya Shilingi Milioni 50 Kwa Ajili ya Kuchangia Harambee ya Kusaidia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lindi Iliyoungua Moto Wiki Iliyopita.

Kwa Kutambua Umuhimu wa Elimu kwa Watoto Shirika Hilo Kupitia Mkurugenzi Mkuu Wake, Aliewakilishwa na Meneja wa Mkoa Bi Nour Aziz Limetoa ahadi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa Alieongoza Harambee Hiyo Ambayo Ilihudhuriwa na Wadau Mbali mbali Akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete

Katika Harambee Hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 80 Taslimu zilichangwa Huku Ahadi na Vifaa vya Ujenzi zikifikia Shilingi Milioni 640 Ambapo Katika Ujenzi Mpya Waziri Mkuu Ameagiza Kujengwa Jengo la Ghorofa litakalokuwa na Ofisi na Madarasa.

Katika Tukio Hilo la Moto, Jumla Ya Madarasa 9 na viti na Meza zaidi ya 300, Ofisi 4 na Vyoo Matundu 24 Viliteketea na Moto Uliotokana na hitilafu ya Umeme
NSSF-Harambee Lindi
Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi,Bi Nour Aziz(kulia)akiwasilisha Ahadi ya Shirika Hilo la Kuchangia Milion 50 Katika Harambee Hiyo Iliyoongozwa Na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.
NSSF-Harambee Lindi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akimshukuru Bw Juma Namuna,Mkuu wa Kitengo cha Mafao Baada ya Shirika Hilo kuahidi Kuchangia Milioni 50.
NSSF-Harambee Lindi
Baadhi ya Vifaa Ikiwemo Saruji Vilivyotolewa na Wadau Mbalimbali Kuchangia Ujenzi mpya wa Shule ya Sekondari Lindi.
NSSF-Harambee Lindi
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete Nae Akiwasilisha mchango wake katika Harambee Hiyo Huku Taasisi ya WAMA Ikihaidi Pia Kuchangia Vitabu Vya Shule Hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top