NIJUZE NIJUZE Author
Title: JOKATE AMWAGIA SIFA KEDEKEDE DIAMOND KATIKA UCHEZAJI WA WIMBO "KIDOGO" ATAMANI AFANYE NGOMA NA ALIKIBA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz anazidi kuwa karibu tena na ma-ex wake. Jacqueline Wolper, Wema Sepetu hawana noma naye tena – na sasa Jokate Mwegelo ! ...
Diamond Platnumz anazidi kuwa karibu tena na ma-ex wake. Jacqueline Wolper, Wema Sepetu hawana noma naye tena – na sasa Jokate Mwegelo!
Jokate Mwegelo
Ya Jokate ina nguvu zaidi kwakuwa kwa sasa ana uhusiano na hasimu wake kiburudani, Alikiba na hiyo ni ishara kuwa uadui kati ya Diamond na Kiba umebaki kwa mashabiki tu.

Mrembo huyo amempongeza Diamond kwa uwezo wake mkubwa wa uchezaji wa style mpya kwenye hit single yake, "Kidogo".
post
Akipost kipande cha video Instagram kikimuonesha Diamond na dancers wake wakifanya mazoezi kwa wimbo huo, Jokate ameandika: 
You just took choreography ya East African tracks to another sphere, inspirational is an understatement. Moves za kwenye huu wimbo. I can’t even hata.”
Jokate pia anatamani amuone Chibu na Kiba kwenye ngoma moja.
“Naendelea kusubiri siku utakayo fanya kazi na team kiba tho- kiroho safi . Hongera kwa kazi nzuri dogo @diamondplatnumz.”

Mapokezi ya post hiyo yana mchanganyiko wa hisia. Ila wengi wamempongeza.

Mara ya mwisho Jokate anamuongelea Diamond ilikuwa ni malalamiko aliyommwagia kwa kumuita mswahili na mdhalilishaji wa wanawake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top