AFANDE SELE ‘AMPASUA’ MBUNGE WA CCM (+Audio)

Afande Sele
“Sikutegemea kuona mtu wa aina ile anakwenda kuongea na kufikia hatua ya kulidhalilisha jeshi kwa sababu mimi ni Mwanajeshi … sasa leo anatokea mbunge from no where, mtu ambaye ubunge wenyewe kaupata kama vile anakabidhiwa chupa ya chai hata haitingishwi na ikitingishwa inapasuka”.

Hilo ni povu lililomtoka Afande Sele baada ya kuulizwa juu ya kile alichokisema Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kuhusiana na ile sanamu ya askari pale Posta.


May 13 mwaka huu akichangia makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mlinga alisema “ingekuwa amri yangu tungechonga sanamu la Diamond tukaliweka kwenye mnara wa askari, ule mnara tumeuchoka … ametufikisha mbali na ameitangaza nchi yetu huko mbele”.

Sasa afande sele kwa kuwa na yeye ni Mwanajeshi hasira zikampanda kuona jeshi linadhalilishwa na mbunge huyo kakaliwa kimya, hivi ndivyo alivyoamua Afande Sele kumpasua mbunge huyo. Imekuaje? Afande Sele anapovuka kama anavyosikika kwenye sauti hapo chini.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post