Wawakilishi pekee nchini katika Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) Yanga SC wameshindwa kutamba mbeli ya wenyeji wao MO Bejaia na Kukubali kipigo cha mapema zaidi Mnamo dakika ya 20 ya Mchezo. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika matokeo yalibaki 1-0.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Yanga kuendelea kutawala mchezo huo lakini hawakuweza kufanikiwa kupata Goli lolote hadi kipenga cha mwisho wa mchezo huo.
Yanga sasa wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi hilo, huku wakiwa hawana goli wala point moja. Mechi inayofuata itachezwa jijini Dar es salaam kwa Yanga kuwakaribisha Tp Mazembe ambayo inaongoza katika Kundi hilo kwa kuwa na jumla ya point 3.
UNAWEZA TAZAMA GOLI WALILOFUNGWA YANGA HAPA.