NIJUZE NIJUZE Author
Title: HII HAPA RATIBA KAMILI YA ZIARA YA KIMICHEZO YA MBEYA CITY NCHINI MALAWI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Siku chache baada ya kumalizika kwa Ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015/16, Ratiba ya mwanzo ya michezo kadhaa ya kirafiki amb...
Siku chache baada ya kumalizika kwa Ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015/16, Ratiba ya mwanzo ya michezo kadhaa ya kirafiki ambayo kikosi cha Mbeya City Fc kitacheza kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya wa 2016/17 imetoka.
Mbeya City Fc
Kwenye ratiba hiyo, City imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka dimbani Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18 kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets, ambapo kwa mujibu wa waandaaji, mchezo unatarajia kushuhudiwa na watazamaji wengi hasa ukizingatia ushawishi wa timu hiyo kwenye soka la nchi hiyo.

Mkuu kitengo cha habari na mawasiliano kwenye kikosi cha City, Dismas Ten , amesema kuwa mchezo wa pili nchini humo utachezwa jijini Lilongwe na utakuwa dhidi ya wenyeji Civo United, kwenye dimba la Civo Stadium hii itakuwa ni Juni 21.


“Baada ya mchezo huo wa pili jijini Lilongwe, tutarudi kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi hiyo, Mzuzu, hapo tutacheza na wenyeji wetu Mzuni Fc, Juni 25 huu utakuwa mchezo wa mwisho kwenye ziara hii ya michezo ya kirafiki, baada ya hapo tutarudi nyumba tayari kwa michezo mingine ambayo imepangwa ukiwemo dhidi ya Simba tutakaocheza Morogoro”


RATIBA YA MICHEZO YA MATAYARISHO YA MSIMU MPYA IKO HIVI:


  • JUNI 18: Big Bullets Vs City - Kamuzu Stadium. 1600hrs
  • JUNI 21: Civo United Vs City - Civo Stadium. 1600hrs
  • JUNI 25: Mzuni FC Vs City – Mzuzu Stadium. 1600hrs
  • JULAI 31: City Vs Simba Sports - Jamhuri. 1600hrs
Kama mambo yatakwenda sawa, ratiba hii inaweza kuwa na ongezeko la michezo miwili ya kirafiki katikati ya mwezi julai kabla ya mchezo wa mwisho wa mwezi huo dhidi ya Simba na mwingine mwanzoni mwa mwezi wa nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.

City inatarajia kuondoka jijini Mbeya Juni 16, kuelekea jijini Blantyre tayari kwa michezo hiyo 3.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top