RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HUU SIKU YA LEO MAY 04, 2016

John Pombe Magufuli
Taarifa kutoka Ikulu May 04 2016 imeeleza kuhusu uteuzi alioufanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, Rais Magufuli amemteua Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani. 

Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Taarifa
Previous Post Next Post