KWA HILI LULU ANATAFUTA KIKI AU NDIO ANAWACHANA WENZAKE WATAFUTA KIKI?

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi wanapenda kiki kuliko kusaka fedha kitu ambacho yeye hakifanyi.
Elizabeth Michael ‘Lulu’
Akizungumza na Lindiyetu.com, pasipo kuwataja majina, Lulu alisema anashangazwa na tabia ya mastaa wengi kuwa ‘bize’ kutafuta kiki kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii badala ya kukutana pamoja na kufikiria ni kitu gani wanaweza kufanya ili waendelee kimaisha.
“Jamani mimi nashangaa siku hizi huku mjini mastaa wanatafuta kiki sana kuliko kufikiria mbinu ya kusaka hela yaani ni shida kabisa, tubadilike jamani, muda unakwenda,” alisema Lulu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post