HUU HAPA UJIO MPYA WA WEUSI, VIDEO YASHUTIWA SOUTH AFRIKA

Ngoma mpya ya kundi la Weusi inaitwa Sweety Mangi, imefahamika.
Joh Makini, G-Nako na Nick wa Pili
Joh Makini, G-Nako na Nick wa Pili walikuwa jijini Johannesburg wiki hii kushoot video kadhaa ikiwemo ya wimbo huo.

Watatu hao wameshare picha kwenye kurasa zao za Instagram wakiwa location ya ndani kushoot video hiyo na muongozaji Justin Campos.

“Sweet mangi video….done….kaamkao wa kula,” ameandika Nick kwenye picha aliyoiweka Instagram.

Sweety Mangi si video pekee waliyoenda kushoot. Kabla ya hapo walishoot video nyingine ya wimbo wa Joh Makini aliomshirikisha staa wa Nigeria, Chidinma. Pia kuna wimbo waliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, Khuli Chana.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post