NIJUZE NIJUZE Author
Title: BAADA YA KUPIGWA STOP SNURA AWASILISHA VIDEO SAFI YA CHURA NA KUWAOMBA WATANZANIA RADHI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Snura na mene...
Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili.
Snura
Snura na meneja wake HK wakiongea na waandishi wa habari Alhamis hii
Snura aliongozana na meneja wake, Hemed Kavu maarufu HK kwenye mkutano na waandishi ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam Alhamis hii.

“Mimi ni meneja wa Snura Mushi, tunaomba radhi kwa umma na Tanzania kwa ujumla kwa kosa la kutengeneza na kuzindua na kuweka mtandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya kitanzania,” alisema HK.

“Aidha tunaomba radhi vyombo vya serikali, vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa shughuli za sanaa hapa nchini. Mimi kama meneja na msanii wangu tunaahidi hatutarudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji, na iwapo tutarudia adhabu kali juu yetu zichukuliwe,” aliahidi HK.

Aliongeza, “Pia naahidi kuwa mfano bora kwa jamii inayotuzunguka, wasanii wenzetu katika kutunza na kufuata maadili na tamaduni zetu pamoja na sheria za nchi. Hii ni pamoja na kufuata sheria katika mamlaka na taasisi, tunafamu kwamba baadhi ya wasanii hasa hasa wa kizazi kipya, hawajajisajili Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama ilivyokuwa kwa msanii wangu, Snura. Lakini kwa sasa baada ya kupata maelekezo kutoka BASATA, Snura ameshajisajili. Pia tunawashauri wasanii kabla ya kufanya video ya wimbo, waende Bodi ya Filamu kwa ajili ya kupata vibali. Mwisho kabisa tunaahidi kutekeleza maazimio na maelekezo yote yaliyotolewa katika kikao cha Wizara. Maagizo hayo ni kutoa video kwenye mtandao wa YouTube na hilo tumeshalitekeleza, kujisajiri BASATA , tayari tumeshajisajili, na tatu ni la kuifanya upya video ya Chura ambapo mpaka sasa tumeshaandaa script na ipo Bodi ya Filamu inakaguliwa na kila kitu kinaenda sawa.”
Jana video na wimbo huo ulifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa la taifa, BASATA.

Kwa upande wake Snura alizungumzia kwanini aliamua kufanya video ya namna ile wakati anajua kufanya hivyo ni kosa.

“Labda nizungumze kitu kimoja, unajua kila mmoja ana upeo wake wa kifikiria, mimi wakati naanza hii video, kwa sababu nilijua ni Chura, na Chura anakaa kwenye maji, nikaona video ifanyike kwenye maji. Lakini baada ya kuiangalia video baada ya kuisha na watu nguo zao zilikuwa zimeloa, nikaona hii video haijakaa vizuri, nikachukua maamuzi ya kutoipeleka kwenye television na kuweka kwenye YouTube nikiwa na imani YouTube siyo sehemu ambayo watoto wanaruhusiwa kwenda. Lakini juzi baada ya kuitwa na Wizara nikaambia sheria ya makosa ya kwenye mitandao, hairuhusu kufanya hivyo, hivyo tunaomba radhi kwa kilichotokea,” alisema Snura.

About Author

Advertisement

 
Top