Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dr. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ana kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.
Kufuatia sakata hilo la kuondolewa kwa nafasi hiyo Lindiyetu.com Ilifanya juhudi ya kumpata mkuu huyo wa zamani wa Mkoa wa Shinyanga na alikuwa na Haya ya Kusema ::>>
“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.
Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
Kufuatia sakata hilo la kuondolewa kwa nafasi hiyo Lindiyetu.com Ilifanya juhudi ya kumpata mkuu huyo wa zamani wa Mkoa wa Shinyanga na alikuwa na Haya ya Kusema ::>>
Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
Tags
HABARI ZA KITAIFA