NIJUZE NIJUZE Author
Title: MVUA ZAONGEZA MAJI BWAWA LA KIDATU NA KUHATARISHA MIUNDOMBINU YAKE
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha kuongezeka kwa maji kupita kiasi katika bwawa la kufua umeme la Kidatu na kuvuka kiwango chake ch...
Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha kuongezeka kwa maji kupita kiasi katika bwawa la kufua umeme la Kidatu na kuvuka kiwango chake cha kawaida cha mita za ujazo 450 hadi 450.5 kutoka usawa wa bahari, hali inayotishia kuharibika kwa miundo mbinu ya bwawa hilo na maji kuwaathiri wananchi wanaofanya shughuli zao zikiwemo za uvuvi na kilimo kandokando ya mto Ruaha mkuu na Kilombero.
 bwawa la kufua umeme la Kidatu

Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme Tanzania Tanesco Mhandisi Felchecim Mramba amesema maji hayo yakiachiwa, yanaweza kusababisha maafa makubwa na hasara kubwa kwa taifa, kwani miundo mbinu itaharibika na uzalishaji wa umeme hautaweza kuendelea, wakati umeme unaotumia maji umekuwa na manufaa makubwa ikilinganishwa na ule unaotumia nishati nyingine na mara ya mwisho hali kama hiyo kujitokeza ilikuwa ni mwaka 2007.

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe na uongozi wa Tanesco wamelazimika kutembelea maeneo hayo na kuamuru kufunguliwa kwa mageti makubwa yaliyojengwa maalum kudhibiti maji, ambayo maji kwa sasa yanalazimika kupita juu yake, jambo ambalo sio salama kitaalamu, huku wananchi wakitakiwa kuchukua tahadhari hasa wakati huu mvua zinapoendelea kunyesha na mkoa wa Morogoro ukiwa ni miongoni mwa mikoa 10 iliyotajwa kupata mvua za juu ya wastani.

Bwawa hilo mwaka jana lilikuwa na maji chini ya mita 433 kutoka usawa wa bahari, kiwango ambacho ni cha chini sana, huku mwaka huu ikielezwa wingi huo wa maji umetokana na maji ya mto Lukosi na Iyovi ya Morogoro pekee huku yale yanayotoka bwawa la Mtera yakiwa yamezuiliwa kwa sasa.

About Author

Advertisement

 
Top