Leo Mapema Mkali wa Bongo Fleva ambaye anaiwakilisha Vyema Tasnia ya Muziki nje ya nchi Diamond Platnumz ameweza kuwashtua Mashabiki wake kwa kutupia Picha katika Ukurasa wake wa Instagram ambayo ikimuonesha kuwa amevaa Kipini katika eneo la Pua yake.

Mashabiki hao waliweza kufika mbali na kuanza kumshambulia Diamond kwa Maneno makali ambayo haya ni Baadhi tu ya yale yaliosemwa:-
kvillahh Acha kuiga ujinga wewe umelelewa kwenye maadil mema na na tamaduni zetu azijafika uko usione side kwa vijisent ulivyopata ukaona akuna may we kukushauli fala wewe utapoteza mashabik na mimi ni mmoja wapo kwani ukiwa simpo u takuaje mpaka muige mbele aya uyo uliyomuiga ukisikia anafilika na wewe so utatamani kufilika badilika acha kuiga ujinga bata mzinga we tandale wew@diamondplatnumz
queen_kajira Mmh...toa hicho jamn hapo umeharibu Sasa khaa!
dullayoreus umezingua jomba apo tena umekua mtoto mchele mchele rasmin
march_boy_1996 Oya jamn huyu sianasema wana H I P wanabana pua nayy amebana nn? Au ameban **** nn?????? Huko anakoelekea ckuzur atakuja kuvaa vikuku atuoneshe
aleezgeneKUANZIA LEO NIMEJIVUA USHABIKI KWAKO NA KU UNFOLLOW ULIMSEMA SANA CHID BEENZ MWAKA 2013 KWENYE WIMBO NA MITAANI YAKATAPAKAA LEO WEWE KUTOKA KIOO CHA JAMII MPAKA MCHAFUZI WA JAMII ...NA SASA UMEFIKA PABAYA NA UTAFIKA PABAYA KIFUPI TU UMEBOA.
Lakini Hapo baadaye Msanii huyo aliweza kuweka Picha nyingine ambayo ilimuonesha akiwa kawaida kabisa bila ya kipini wala kitobo katika sehemu ya Pua yake na kuandika hili:-

diamondplatnumzJus woke up like😴.... guess what??? Jus few days to go...i can't wait for our Reality Show to get aired...😜 #FromTandaleToTheWorldTourHaikuishia hapo tu Meneja wake Babutale naye aliweza kutoa tamko lake juu ya Picha hiyo ya Mwanzo wa Msanii wake naye alisema kuwa Usiamini kila ukionacho kwenye Picha au kwenye TV
Tags
HABARI ZA WASANII