Msanii kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chingunda amesema anatamani Kundi la TMK Wanaume Family lirudi kama zamani hata sasa hivi.

Akizungumza katika kipindi cha Mkasi cha East Africa Television Jumatatu hii, Chege alisema kuwa Rais Kikwete aliwaambia kuwa amehuzunishwa sana na kitendo cha kundi hilo kuvunjika kwani alikuwa akiona jinsi ambavyo walikuwa wamefanikiwa.
“Kiukweli kabisa mimi mwenyewe na kila mtu anatamani kundi la TMK Wanaume Familiy lirudi kama zamani hata sasa,” alisema Chege.
“Sababu kuna vitu tulikuwa tukifanya navikumbuka sana, na siamini kama kuna mtu ndani ya kundi lile ambaye hapendi hicho kitu kitokee. Kuna wakati mpaka tuliitwa na Rais Jakaya Kikwete ili aweze kutuweka sawa turudi kama zamani sema mwenzetu mmoja hakuweza kutokea” alifafanua zaidi Chege.
Katika hatua nyingine Chege amekiri kuwa Juma Nature ndiye alikuwa msanii mkubwa kwenye kundi hilo na ndiye aliyeweza kuwaweka wao kwenye ramani ya muziki wa bongo fleva mpaka kufikia hatua ya kufanya vyema na kukubarika kwa jamii.

Tags
HABARI ZA WASANII