Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa Halmashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesisitiza fedha za Elimu ambazo zimetolewa na Serikali kama zawadi katika Halmashauri mbalimbali zilizofanya vizuri katika Sekta ya Elimu zitumike vizuri.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati wa kutoa zawadi kwa Halmashauri 10 ambazo zimepokea Shilingi Bilioni 15.5.
Halmashauri hizo ni Mbinga, Chato, Busega, Lushoto, Niyankasi, Liwale, Sikonge, Mbarali, Mpanda, pamoja na Tabora.
Pia, Profesa Ndalichako amezitaja Halmashauri 10 za mwisho kuwa ni Rombo, Kiteto, Meatu, Mafinga, Kasulu, Butihama, Wanging’ombe, Mbozi na Makambako.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.George Simbachawene amezitaka Halmashauri hizo ambazo zimefanya vizuri na kupata zawadi hiyo ya fedha kuzitumia vizuri fedha hizo na kuhakikisha Elimu Bora inapatikana.
Tags
HABARI ZA KITAIFA