
Stars inayonolewa na kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa “Master” ilifunga bao hilo dakika ya 30 kipindi cha kwanza na likadumu hadi mapumuziko na timu ziliporejea zilicheza na kutoshana nguvu hivyo stars ikabaki na ushindi huo.
Bao hilo limeisaidia Stars kuifikia Nigeria kwenye msimamo wa kundi G kwa alama 4 baada ya michezo 3 na itawasubiri Chad kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa taifa Dar es salaam.
Mchezo wa mapema ulikuwa ni kati ya Benin na Sudan Kusini ambapo Benin wameshinda bao 2 kwa 1.
Matokeo ya Michezo mingine ni kati ya Guinea Bissau na Kenya, Kenya wameshindwa kutamba mbele ya Guniea Bissau kwa kukubali kichapo cha bao moja wakati Zambia na Congo wametoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana huku Libya ikikubali nayo kichapo cha goli 2 kwa moja licha ya kuanza kuongoza katika kipindi cha kwanza bao moja dhidi ya Sao Tome.
Tags
SPORTS NEWS