Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema atamwiga Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kushughulikia masuala ya ufisadi na uzembe kazini katika nchi yake.

Kagame ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wote wa serikali katika kuwakumbusha wajibu wao katika kuwatumikia wananchi wa Taifa hilo.
Wakati huo huo Rais Kagame ameelezea kusikitishwa kwake na Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya mikutano ya mara kwa mara na kusafiri kila mara jambo ambalo linaiumiza serikali yake katika suala la matumizi.

Aidha katika hotuba yake Rais Kagame ameeleza kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli katika kuhakikisha taasisi za serikali nchini mwake zinafuata miiko na maadili ya kazi za umma na kuwaasa wote ambao wanajihusisha na utovu wa nizamu kazini na ufisadi kwamba hatawavumilia.
Tags
HABARI KIMATAIFA