NAY WA MITEGO ASHAMBULIWA HADI KUVUNJIWA KIOO CHA GARI YAKE, MKASA MZIMA HUU HAPA

Nay wa Mitego
Msanii wa Bongo Fleva Nchini Nay wa Mitego amekumbana na Kadhia ya Kuvunjiwa Kioo Cha Nyuma cha Gari yake wakati akielekea kwenye Utambulisho wa Video yake Mpya ya "SHIKA ADABU YAKO" katika Kipindi cha FNL (Friday Night Live) Kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.

Nay wa Mitego ameweza kushare nasi Habari hii na kuandika haya kwa Masikitiko makubwa kabisa kwani Tukio hili lilimfanya ashindwe kufika kwenye kipindi hicho na Kutambulisha kazi yake hiyo.
Nay wa Mitego
Nay aliandika Haya kwenye ukurasa wake wa Instagram::
Nimevunjiwa kio Cha gari nikiwa njia naenda kwenye Intrvw Chanel5 EaTv kwa ajili ya kutambulisha my New Video #ShikaAdabuYako sorry Watu wangu mliokua mkisubiri kuona Video Na Intrvw yote nimeshindwa kufika naweka sawa ili. Video itaenda YouTube kesho itakua kwenye Tv yako Pendwa. Muziki sio vita..... I will never stop doing what i do.!!
Previous Post Next Post