MANCHESTER UNITED USO KWA USO NA LIVERPOOL UEFA EUROPA LIGI.

Manchester United wamepangwa kucheza na Liverpool kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
UEFA EUROPA LIGI.
Droo ya Raundi hii imefanyika Jana Mjini Nyon, Uswisi.
Mechi za kwanza za Raundi hii zitafanyika Alhamisi Machi 10 na Marudiano ni Machi 17. Man United wataanzia Ugenini huko Anfield na kumalizia kwao Old Trafford.

Msimu huu Man United na Liverpool zishakutana kwenye Ligi Kuu England na Man United kushinda Mechi zote mbili, 3-1 ndani ya Old Trafford na 1-0 huko Anfield.

Timu nyingine ya England ambayo ipo hatua hii ni Tottenham ambayo imepangwa kucheza na Borussia Dortmund ya Germany.

EUROPA LIGI -DROO YA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16

KALENDA
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel
Previous Post Next Post