Rais Magufuli ameamuru kurudi nyumbani mabalozi wawili haraka akiwemo Dr Batilda Buriani, Dr James Nsekela wa Italia na Peter Kalaghe wa Uingereza.
Pia Mkurugenzi mkuu wa NIDA Bw Mwaimu amesimamishwa kazi kuanzia sasa kupisha uchunguzi wa Bilioni 179.6.
Akitangaza hatua hiyo, Katibu mkuu kiongozi Ombeni sefue amesema Batilda na mabalozi wengine watano wamekuwa hawafanyi kazi kikamilifu ya kuiwakilisha nchi kama jinsi majukumu yao yanaavyoeleza.
Sefue amewataka mabalozi hao watatu kuondoka leo hii katika nchi waliko na kurudi Tanzania.
Kuhusu Mwaimu, Sefue amesema yeye na vigogo wengine watatu wa NIDA wameaimamishwa kazi mara moja.
Aidha Rais Magufuli amemfukuza kazi Katibu Tawala mkoa wa Katavi Madeni Kipande kwa kushindwa kazi na Rais kutokuridhishwa na utendaji kazi wake.
Kipande aliteuliwa na JK kuwa katibu tawala Mkoa wa Katavi wiki moja kabla ya Magufuli Kuapishwa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa NIDA, katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
Picha Michuzi Jr-MMG