
Daraja hilo linalojengwa kwa ubia kati ya serikali na mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF litakuwa na urefu wa kwenda juu (Vertical) mita zaidi ya 680 wakati urefu mlazo (Horizontal) utakuwa zaidi ya kilomita 2.
Daraja hilo la kuning'inia (Cable-stayed bridge) linajengwa na kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company kwa gharama ya dola za Kimarekani 136 milioni.

Lilianza kujengwa Februari 2012 na linatarajiwa kumalizika mwaka huu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA