KIVUKO CHA MTO KILOMBERO CHAZAMA, ABIRIA ZAIDI YA 29 WAOKOLEWA

Kivuko
Kivuko cha mto Kilombero mkoani Morogoro kimezama kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari yapatayo matatu

Habari kutoka Kilombero zilizothibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Leph Gembe zinadai kuwa ajali hiyo imetokea jana Majira ya saa 1 usiku wakati kivuko hicho kikitokea Ulanga.

Alisema kuwa Jumla ya watu zaidi ya 30 ndio walikuwepo katika kivuko hicho na kuwa jitihada za uokoaji zilifanyika na watu zaidi 29 waliokolewa

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni upepo Mkali na mawimbi makali yaliyopelekea kivuko hicho kuzama na kuwa hadi sasa bado taarifa kamili kupatikana na pindi atakapopata habari kamili atazitoa

Mkuu huyo alisema kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Daraja
Muonekano wa Misingi ya Daraja la Mto huo, huku kivuko kilichozama kikionekana kulia.
Kivuko
Previous Post Next Post