Mgogoro wa kisiasa na kisheria ulioikumba Zanzibar tangu kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba ukiendelea, hapo jana Rais Ali Mohammed Shein wa Chama cha Mapinduzi, CCM, alisema yeye bado ni rais halali wa Zanzibar kwa mujibu wa Katiba na wanaopingana na hilo wafungue shauri mahakamani.
Kauli hiyo imeshitua wengi na hapa mwanasheria Fatma Karume anaeleza mtazamo wa kisheria wa kauli kama hii.