FM ACADEMIA WAACHA HISTORIA MKOANI LINDI KWA TUKIO HILI HAPA.

FM ACADEMIA SHOW LINDI
Bendi ya FM ACADEMIA wa zee wa Ngwasuma Jana Jumamosi ya tarehe 9/01/2016 waliweza kutoa burudani ya nguvu kwa Wakazi wa Mji wa Lindi na Vitongoji vyake katika Ukumbi wa Hoteli ya Kisasa kabisa Lindi Beach Resolt.

Bendi hiyo ilifanya show hiyo mkoani hapa kwa Udhamini wa Mashujaa FM Radio iliweza kutimiza kile kilichotarajiwa na wengi kutokana na Umahiri wake wa kufanya Show ya Live kwa Ustadi wa Hali ya juu.
FM ACADEMIA SHOW LINDI
Ikiongozwa na Kiongozi wake Nyoshi El Sadat aliambatana na waimbaji na Marapa wote wa Bendi hiyo na kufanya Show hiyo kuwa yenye Mvuto wa pekee pia Madancer wake waliweza kutoa Show ya nguvu.
FM ACADEMIA SHOW LINDI
Mmoja wa Mashabiki wa FM ACADEMIA aliohudhuria Show hiyo ameiambia LindiYetu.com Kuwa wameweza kufurahia weekend yao Vizuri kwa Show kali ya bendi hiyo.

Pia akiwapongeza Mashujaa FM Radio kwa kuwaletea Burudani hiyo na Pia aliwaomba kuendelea kuwaletea Burudani Nyingi zaidi kwani Kusini sasa Inaongea.
FM ACADEMIA SHOW LINDI
Bendi hiyo Leo hii itakuwa Mjini Masasi kuwapa Burudani wakazi wa Mji huo.
 
Patcho Mwamba akimchezesha Mmoja wa Wadau na Mashabiki wakubwa wa Bend ya FM Academia Mkoani hapa Lindi.
FM ACADEMIA SHOW LINDI 
Wapenzi na Wapenda Burudani wa Mkoa wa Lindi walifurika katika Ukumbi wa Hoteli ya LindiBeach Resolt kushuhudia Show kubwa kabisa kutoka kwa FM ACADEMIA iliyofanyika Jumamosi ya Tarehe 9/01/2016.
FM ACADEMIA SHOW LINDI

 
Hahika ilikuwa Patashika Nguo kuchanika Ndani ya Lindi Beach Resolt Jumamosi ya Terehe 9/01/2016 katika Show ya Fm Academia wazee wa Ngwasuma ilipokuwa ikitoa Burudani live ndani ya Mkoa wa Lindi.
 
FM ACADEMIA SHOW LINDI 
Mtangazaji na mmoja walioandaa na Kuhakikisha mambo yanakwenda Sawa katika Show hiyo Juma Diwani akitoa neno la shukrani kwa wadau na Mashabiki wa 89.3 Mashujaa Fm na Fm Academia kwa kuhudhuria Show hiyo, Pia aliwaambia wawemkao wa Kula mambo mengi mazuri Yanakuja.
 FM ACADEMIA SHOW LINDI 
Wadau wa Mtandao wa LindiYetu.com Wakiwa wamejiachia na Camera yetu iliyokuwa ndani ya Viwanja Hivyo. Hakika iliandikwa Historia ya Kiburudani na Wazee wa Ngwasuma.
Previous Post Next Post